Kitaifa

Wazee Simba sasa kukimbilia Mahakamani

on

BARAZA la wadhamini la klabu ya Simba limetishia kwenda mahakamani kuzuia mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 13 hadi hatma ya viongozi wakuu wa klabu hiyo wanaoshikiliwa na vyombo vya dola ijulikane.

Rais wa klabu hiyo Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange ‘Kaburu’ wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za utakatishaji fedha ambapo wapo rumande kwa zaidi ya mwezi sasa.

Katibu wa baraza hilo, mzee Hamis Kilomoni amesema haoni sababu ya kufanyika kwa mkutano huo kwa uharaka huo huku viongozi wao wakiwa rumande hivyo amewataka wanaokaimu kusitisha zoezi hilo mpaka itakapofahamika hatima ya viongozi hao.

Rais Evans Aveva akiingia mahakama ya Kisutu

“Tunataka uongozi unaokaimu kusitisha zoezi la mkutano mkuu na endapo watakaidi tutakwenda mahakamani kwakua huko ndiko kuna haki zaidi, sijaona haja ya kufanya jambo hilo kwa haraka hivyo” alisema Kilomoni.

Moja ya ajenda ambayo imepangwa kujadiliwa kwenye mkutano huo ni mabadiliko ya katiba ambayo yakipitishwa yataruhusu uendeshwaji wa klabu hiyo kwa njia ya hisa ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ anataka kuwekeza asilimia 51.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *