Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Yanga, Mtibwa Kupigwa Jamhuri Kama Kawa

0 22
Related Posts
1 of 948
Sheila Ally, Dar

MECHI ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga iliyokuwa inadaiwa kutochezwa Uwanja wa Jamhuri mjiji Morogoro sasa itachezwa kwenye Uwanja huo huo na kwa muda uliopangwa wa Machi 4. 


Hivi karibuni Shirikisho la Soka nchini (TFF) lilitangaza kuufunga uwanja huo lakini Meneja wa Uwanja, John Simkoko amesema kuwa hakuna marekebisho ya mechi za ligi kuu kutochezwa hapo kwani marekebisho wanayofanya ni madogo.


Mkoko alisema kuwa hata katika barua yao kwenda TFF haikuekeza kufungwa kwa uwanja kwani hadi sasa mechi za ligi daraja ka kwanza (FDL) na ligi daraja la pili (SDL) zinaendelea kuchezwa hapo na zitamalizika Februari 10.


“Tunaamini hadi Machi marekebisho yetu yatakuwa yamekamilika kwani ni madogo tu hivyo mechi ya Mtibwa Sugar na Yanga itachezwa hapa. Marekebisho tutayaanza hizi mechi za SDL na FDL zitakapomalizika mwezi ujao hivyo tutakuwa na mwezi mzima wa kurekebisho, kikubwa mvua isinyeshe.


“Wengi wamechukulia hili suala kwa mtazamo wa tofauti kana kwamba Simba hawajatendewa haki lakini sio hivyo kwa maana kwamba uwanja haujafungwa ni marekebisho madogo tu,” alisema Simkoko.


Simkoko alifafanua pia kuwa wasingeweza kufunga uwanja huo kwa mechi za ligi za SDL na FDL wangekosa sehemu ya kuchezea.


“Mtibwa wana uwanja wao na hapa Jamhuri ni mechi mbili tu za ligi zinachezwa ambazo ni Simba na Yanga wanapokuja kucheza hapa Morogoro lakini kuna hawa vijana wetu wasiokuwa na uwezo kifedha wangeenda kutumia uwanja gani kama huu unafungwa,” alihoji Simkoko.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...