The sports Hub

Yanga Yatisha Tuzo za TPL Novemba

0 181

MATOKEO mazuri waliyoyapata Yanga hivi karibuni yamepelekea kocha Mwinyi Zahera na straika Heritier Makambo watwae tuzo za Ligi Kuu Tanzania kwa mwezi Novemba.

Kamati ya tuzo imemchagua kocha Zahera kuwa Kocha Bora wa Novemba akiwashinda kocha mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda na kaimu kocha mkuu wa Alliance FC, Gilbert Dadi alioingia nao fainali.

Kamati hiyo pia imemchagua Makambo kuwa mchezaji bora wa Novemba akiwashinda wenzake wawili, Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ wa Yanga.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.