Kitaifa

Yanga Yawafuata Chui wa Kenya SportPesa

on

TIMU ya Yanga imeungana na AFC Leopards ya Kenya katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Tusker FC kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru.

Yanga waliweza kuwamudu vizuri Tusker katika dakika 30 za mwanzo na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Tusker lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya nahodha Situma James ilikuwa imara kupitika.

Tusker ambao asilimia kubwa ya wachezaji wake wana maumbo makubwa waliweza kuhimili kashikakashi za vijana wa Jangwani huku mshambuliaji wao Alan Wanga ambaye aliwahi kuichezea Azam FC akikosa mbinu za kuipita safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya nahodha Nadir Haroub.

Yanga walifunga penalti zao kupitia kwa Nadir, Obrey Chirwa, Maka Edward na Said Musa huku Wahula Noah na Brian Osuma wakifunga kwa Tusker wakati Owusu Stephen na Alwanga wakikosa mikwaju yao.

Katika mchezo huo benchi la ufundi la Yanga lilikuwa chini ya kocha msaidizi Juma Mwambusi kutokana na kocha mkuu George Lwandamina kuwa mapumzikoni nchini Zambia.

Yanga iliwatoa Emmanuel Martin, Juma Mahadhi na Yusuph Mhilu nafasi zao zikichukuliwa na Said Mussa, Samwel Greyson na Bakari Athuman.

Kwa upande wa Tusker iliwaingiza Wahula Noah, Alwanga Clifford na Owusu Stephen kuchukua nafasi za Moses Ndawula, Michael Khimat na Martin Kiiza.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *