Burudani

Zari amuaga mama yake kwa ujumbe mzito

on

MAMA mzazi wa mpenzi wa Mwanamuziki wa Bongo Flava Diamond Platinum, Zarihina Hassan ‘Zari the boss Lady’ amefariki dunia alfajiri ya leo akiwa na miaka 57 nchini ya Uganda.

Mama Zari alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Nakasero kwa wiki moja kabla ya kifo chake kilichotokea leo akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari alitangaza kifo cha mama yake kwa kuandika maneno yafuatayo:

“Ni huzuni kubwa kwa familia yangu, Ninatangaza kifo cha mpendwa mama yetu kilichotokea leo asubuhi. Roho yake ipumzike kwa amani, Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na kumuweka mahala pema peponi.

“Utaendelea kupendwa na wajukuu zako, sisi watoto wako tunakuombea Mungu akupokee vizuri mama yetu. Tunatambua mchango wako mkubwa kwetu.Tutaendelea kukuombea Mama yetu. Pumzika kwa amani”.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *